Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki ameahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo kisheria baada ya kuteuliwa kuwa msaidizi wa Rais William Ruto.
Akihutubu punde baada ya kula kiapo, Prof. Kindiki amemshukuru Rais Ruto kwa uteuzi huo akisema kuwa amekuwa mwanafunzi wa kisiasa wa Ruto kwa takriban miaka 20 na ana imani ya kutendakazi inavyostahiki.
Kindiki pia amewashukuru wote waliomlea kisiasa, walimu wake na familia yake pamoja na wote waliojitolea mhanga katika kumnoa makali katika ulingo wa siasa.
Ameongeza kuwa uteuzi wake ni ishara ya ukuaji wa demokrasia ya Kenya.