Rais wa klabu ya Young Africans maarufu kama Yanga nchini Tanzania, Hersi Said amechaguliwa mwenyekiti wa kwanza wa chama cha vilabu vya Africa – ACA.
Said ambaye ni kinara wa CECAFA baina ya vilabu alichaguliwa kufuatia uchaguzi ulioandaliwa jijini Cairo nchini Misri, ukiongowza na Rais wa shirikisho la kandanda Afrika Dkt. Patrice Motsepe siku ya Alhamisi.
Said atasaidiwa na manaibu wawili Jessica Motaung kutoka klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Paul Bassey wa timu ya Akwa United ya Nigeria.