Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Kenya-Harambee Stars Francis Kimanzi ametaja kikosi kitakachoshiriki mashindano ya kuwania kombe la Mapinduzi kisiwa Zanzibar mapema mwezi ujao.
Kimanzi amemtema kipa mzoevu Patrick Matasi, akiwaita Byrne Omondi,Farouk Shikalo na Sebastien Wekesa.
Mabeki ni pamoja Brian Okoth,Hanif Wesonga,Charles Momanyi,Alphonce Omija,Silvester Owino,Abud Omar,Ronney Onyango,Siraj Mohammed,Baron Ochieng,Ronald Shichenje na Daniel Sakari.
Wachezaji wa kiungo ni Chris Erambo,Marvin Nabwire,Brian Musa,Michael Mutinda,Boniface Muchiri,Ben Stanley Omondi,Brian Michira,Eric Ovella,David Okoth,Isaac Omweri,James Kinyanjui,Samuel Kapen,Darius Msagha.
Washambulizi ni Ryan Ogam,Francis Kahiro,Beja Nyamawi,Sydney Lokaale na Moses Shumah.
Kikosi hicho kitaripoti kambini tarehe 28 mwezi huu kwa maandalizi, kabla ya kikosi cha mwisho kutajwa kwa mashindano ya kombe la Mapinduzi.
Mashindano hayo yataandaliwa kisiwani Zanzibar kati ya Januari 3 na 13 mwaka ujao, yakiwa matayarisho ya mwisho ya Kenya, kabla ya makala ya nane ya mashindano ya kombe la CHAN.
Mataifa yatakayowania Kombe la Mapinduzi ni pamoja Uganda,Tanzania bara,Burkina Faso,Burundi na wenyeji Zanzibar.
Kenya,Uganda na Tanzania zimeteuliwa kuandaa kipute cha kombe la CHAN kati ya Februari mosi na 28 mwaka ujao.