Kikosi cha raga kitakachowania kombe la Barthes nchini Zimbwawe chatajwa

Tom Mathinji
1 Min Read
kikosi cha wachezaji 28 kitakachoshiriki mashindano ya mwaka huu ya bara Afrika ya kuwania kombe la Barthes yatakayoandaliwa tarehe 20 hadi 28 mwezi huu mjini Harare, Zimbabwe.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 Simon Jawichre, amekitaja kikosi cha wachezaji 28 kitakachoshiriki mashindano ya mwaka huu ya  bara Afrika ya kuwania kombe la Barthes yatakayoandaliwa tarehe 20 hadi 28 mwezi huu mjini Harare, Zimbabwe.

Edmond Omondi atakiongoza kikosi hicho akiwa nahodha pamoja na Geylord Ngasi, Andycole Omollo, Iddo Kuta na Wycliffe Ogutu miongoni mwa wachezaji wengine. Michuano ya mwaka huu itashirikisha timu nne zikiongozwa na wenyeji Zimbabwe, Kenya, Namibia na Tunisia.

Timu hizo zitamenyana kwa  siku tatu huku timu itakayomaliza ya kwanza ikishinda taji hiyo ya  Barthes na kufuzu kuwakilisha Afrika katika  mashindano ya Raga Duniani kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka ishirini kuanzia tarehe 2 hadi 7 mwezi  Julai nchini Scotland.

Timu ya taifa itaondoka humu nchini Alhamisi hii kabla ya kushirki mchuano wao wa ufunguzi dhidi ya Namibia siku ya Jumamosi na kisha  kumenyana na Tunisia Jumatano wiki ijayo kabla kuhitimisha ratiba dhidi ya  wenyeji na mabingwa watetezi Zimbabwe tarehe  28 mwezi huu…

Share This Article