Kikosi cha mwisho cha Wanariadha wa Kenya kuwasili kesho kutoka Tokyo

Dismas Otuke
1 Min Read
Tokyo WCH 2025

Kikosi cha mwisho cha Kenya kinachowajumuisha wanariadha 48 kinatarajiwa kuwasili nchini Jumanne Adhuhuri kutoka Tokyo, Japan, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye mashindano ya kuwania ubingwa wa riadha Duniani.

Miongoni mwa wanariadha watakaowasili kesho kwa ndege za Qatar na Emirates ni pamoja na mabingwa wa dunia Emmanuel Wanyonyi (mita 800), Beatrice Chebet (mita 5,000 na 10,000), Faith Kipyegon (mita 1,500), na Lilian Odira (mita 800).

Wanariadha watakaosafiria ndege ya Qatar Airways watawasili saa saba na dakika 40, huku wale watakaotumia ndege ya Emirates wakitua uwanja wa JKIA saa nane unusu adhuhuri.

Kenya ilimaliza ya pili duniani kwa medali 11 (dhahabu 7, fedha 2 na shaba 2).

 

Website |  + posts
Share This Article