Kikosi cha Malkia kufuzu kwa michezo ya Afrika chatajwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Voliboli kwa vidosho maarufu kama Malkia Strikers kimetangazwa huku idadi ya wachezaji ikipunguzwa kutoka 19 hadi 16.

Timu hiyo iliyotangazwa na kocha mkuu Japheth Munala siku ya Jumatatu inawajumuisha wachezaji wenye tajriba na wasio na tajriba.

Baadhi ya wanandinga waliotemwa kikosini ni joy Lusenaka,Pauline Mishel na Sarah Namisi.

Timu hiyo itaongozwa na nahodha Mercy Moim.

Kikosi kamili kinawajuisha :-

Maseta
1.Emmaculate Nekesa
2.Esther Mutinda

Libero
3.Agripina kUNDU
4.Lincy Jeruto
5.Elizabeth Wanyama

Opposite Players
6.Loice Simiyu
7.Mercy Iminza

Middle Blockers
8.Edith Mukuvilani
9.Lorine Chebet
10.Trizah Atuka
11.Belinda Barasa

Outise Hitters
12.Mercy Moim
13.Jemimah Siangu
14.Juliana Namutira
15.Pamela Adhiambo
16.Pamela Jepkirui

Kenya italenga kutetea taji iliyonyakua mwaka 2019 nchini Morocco.

Share This Article