Ujumbe wa kwanza wa wanariadha wa Kenya watakaoshiriki michezo ya Olimpiki kwa walemavu umewasili mapema Alhamisi jijini Paris, Ufaransa.
Michezo yao ya Olimpiki itaandaliwa kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.
Kenya itashiriki michezo saba ya fani za upigaji makasia, riadha, Taekwondo na uendeshaji baiskeli.
Timu hiyo inawashirikisha wanariadha watano, wanawake wawili na mwanamume mmoja, wachezaji taekwondo wawili, mpigaji makasia mmoja na mwendeshaji baiskeli mmoja.