Kocha mmkuu wa timu ya Kenya kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka 23, Emerging Stars Anthony Kimani ametaja kikosi cha awali cha timu itakayoshiriki raundi ya pili ya kufuzu kwa fainali za Kombe la AFCON dhidi ya Côte d’Ivoire,mwezi ujao.
Kenya itaandaa mkondo wa kwanza Novemba 11 katika uwanja wa Nyayo kabla ya kuzuru Abidjan,katika mchuano wa marudio tarehe 17 mwezi ujao uwanjani Félix Houphouët-Boigny.
Emerging Stars walifuzu kw araundi ya pili baada ya kuwatema nje Tanzania jumla ya mabao 5-4 .
Kikosi kilichotajwa
Makipa
Caleb Kramer, Collins Omondi, Kevin Oduor, Bernard Jairo
Mabeki
Ian Omondi, Joseph Bate, Jackson Imbiakha, Robinson Musungu, Collins Ochieng, Baron Ochieng, Price Musebe, Wyclliffe Awiko, Bilal Otieno, Telena Ochieng
Viungo
Aldrine Kibet, Kevin Wangaya, Kelly Madada, Andres Odhiambo, Irad Mshindi, Humphrey Aroko, Oliver Majaka, Zachary Nyakwara, Glen Githinji, Ateek Omar, Jack Steel, Mark Kithome.
Washambulizi
Brooklyn Kazungu, Lawrence Okoth, Paul Osama, Jeremy Bisau, Syphas Otieno, Stephen Omondi, Dan Omalla, Emmanuel Osoro, Collins Okello, Henry Omollo, Colin Akeno, Javan Ochieng, Hassan Beja
Mshindi wa jumla wa mechi hiyo atafuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao pamoja na tiketi ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.