Kifaa cha mawasiliano cha ndege ya AMREF iliyoanguka chapatikana

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yaanzisha uchunguzi wa ajali ya ndege ya AMREF, iliyotokea Mwihoko.

Chombo cha kunakili mawasiliano ya rubani cha ndege ya shirika la AMREF iliyoanguka huko Mwihoko kaunti ya Kiambu maarufu black Box kimepatikana huku maofisa kutoka wizara ya uchukuzi wakitarajiwa kukitumia kubaini kiini cha ajali hiyo.

Akizungumza na wanahabari huko Mwihokohapo jana, mkurugenzi wa idara ya uchunguzi wa ajali za ndege Fred Kabunge, alithibitisha kupatikana na chombo hicho muhimu. Alisema combo hicho awali kilikuwa kimechukuliwa na maofisa wa polisi kutoka sehemu ya mkasa huo ambao hawakujua umuhimu wake.

Maafisa wa idara hiyo wanatarajiwa kukituma chombo hicho katika mataifa ya Ng’amba ili kusaidia kubaini yaliyomo kutoka kwa washirika wa kimataifa wa uchunguzi wa safari za ndege.

Aidha alisema uchunguzi kuhusu ajali hiyo umeshika kazi huku wapelelzi wakiwahoji waathiriwa.

Share This Article