Kevin Kang’ethe akanusha mashtaka ya mauaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa mauaji Kevin Kang’ethe, awasili Marekani kufunguliwa mashtaka.

Mshukiwa wa mauaji Kevin Kang’ethe, aliyesafirishwa kutoka Kenya kuelekea Marekani siku ya Jumapili, amenyimwa dhamana baada ya kukanusha mashtaka ya mauaji dhidi yake.

Kang’ethe anadaiwa kumuua mpenzi wake Margaret Mbitu, nchini Marekani mwaka 2024.

Kupitia kwa taarifa kutoka afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma, Kang’ethe alifikishwa katika mahakama ya Suffolk Superior, Boston Septemba 3, 2024.

“Mahakama imeamua kuwa atazuiliwa bila dhamana,” ilisema afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa Kang’ethe na Margaret walikuwa katika uhusianio wa kimapenzi, kabla ya mauaji hayo kutokea. Kesi hiyo itatajwa Novemba 5, 2024.

Kang’ethe alitorokea nchini Kenya baada ya kudaiwa kumuua mpenzi wake, ambaye mwili wake ulipatikana ndani ya gari katika uwanja wa ndege wa Logan, Boston Marekani.

Share This Article