Kesi ya tatu yawasilishwa mahakamani kupiga breki ujenzi wa kanisa Ikulu

Kesi hiyo inayopinga ujenzi wa kanisa la shilingi bilioni 1.2 ambalo Rais Ruto alitangaza mwezi jana kuwa unafadhiliwa na pesa zake za kibinafsi na michango ya kirafiki inasubiri uamuzi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kesi ya tatu imewasilishwa katika Mahakama Kuu kupinga ujenzi wa kanisa katika Ikulu ya Nairobi.

Mashirika mengi ya kijamii yanaitaka Mahakama kusitisha hatua ya Rais William Ruto kujenga kanisa katika Ikulu ya Nairobi, yakisema kuwa anakiuka kipengele cha nane cha katiba ya Kenya, kinachomtaka Rais na Ikulu kujitenga na kuwa na dini ya serikali.

Mashirika ya Transparency International Kenya, Tume ya Haki za Kibinadamu nchini, Inuka Kenya ni Sisi na taasisi ya uwajibikaji zinataka pia mahakama kumzuia Rais na maafisa wa serikali kufadhili ujenzi wa kanisa hilo.

Kesi hiyo inayopinga ujenzi wa kanisa la shilingi bilioni 1.2 ambalo Rais Ruto alitangaza mwezi jana kuwa unafadhiliwa na pesa zake za kibinafsi na michango ya kirafiki inasubiri uamuzi.

Website |  + posts
Share This Article