Kesi ya kupinga sheria ya fedha ya mwaka 2023 kusikilizwa leo

Marion Bosire
1 Min Read

Mahakama kuu leo, inatarajiwa kusikiliza kesi dhidi ya utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka huu iliyowekwa na Seneta wa Kaunti ya Busia Okiya Omtata.

Wiki iliyopita, mahakama hiyo iliongeza muda wa agizo la kuzuia utekelezaji wa sheria hiyo mpya kwa siku tano zaidi.

Okiya Omtatah anapinga utekelezaji wa sheria hiyo ya fedha kwa misingi kwamba bunge la Seneti halikuhusishwa katika mpango wa kupitisha sheria hiyo tata.

Omtatah pia aliweka kesi nyingine ya kudharau mahakama dhidi ya mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli – EPRA kwa kile alichokitaja kuwa hatua ya mamlaka hiyo ya kutekeleza ushuru mpya uliopendekezwa kwa sheria ya fedha ya mwaka 2023 ilhali mahakama imesimamisha utekelezaji wa sheria hiyo.

Rais William Ruto, alitia saini mswada wa fedha wa mwaka 2023 Jumatatu Juni 26, 2023 na kuufanya kuwa sheria.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *