Kesi ya kupinga sheria ya fedha mwaka 2023 kusikizwa kwa siku ya mwisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Kesi inayopinga utekelezwaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023 itasikizwa leo Alhamisi na mahakama kuu kwa mara ya mwisho.

Majaji walianza kusikiza kesi hiyo jana Jumatano huku pande zote za walalamishi na washtakiwa zikitoa hoja zao.

Kwenye kesi hiyo, walalamishi wanadai sheria hiyo ilikiuka sheria kwa kufanyiwa marekebisho na kupitishwa bila kuzingatia maoni ya umma.

Sheria ya fedha ya mwaka 2023 ilijumuisha matozo mapya na kuongeza kwa ada ya matozo yaliyokuwepo, hali ambayo imechangia kuongezeka kwa gharama ya maisha.

Baada ya kusikizwa, majaji wanatarajiwa kutathmini uwasilishi wa pande zote kabla ya kutoa uamuzi mwezi Novemba mwaka huu.

Sheria mpya ya fedha ya mwaka 2023 ilianza kutekeleWa rasmi Agosti mosi mwaka huu na ilijumuisha miongoni mwa matozo mengine, ushuru wa nyumba wa asilimia 1.5 ya pato la jumla kwa kila mfanyakazi.

Share This Article