Kenya, Ujerumani na Austria zatia saini makubaliano kuhusu ajira

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto aongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Katika juhudi za kuhakikisha wakenya zaidi wanapata ajira katika nchi za ughaibuni, serikali ya Kenya imetia saini makubaliano kuhusu leba na Ujerumani na Austria.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulioongozwa na Rais William Ruto leo Alhamisi, uliarifiwa kuwa wizara ya leba imetambua nchi kadhaa ambapo Wakenya wanaweza pata ajira, zikiwemo  Australia, Qatar, Canada, Saudi Arabia, Oman, Muungano wa Milki za Kiarabu (UAE), Uingereza, Kuwait, na Ireland Kaskazini.

Baraza hilo la Mawaziri liliarifiwa kuwa ajira hizo zinajumuisha wataalam, walio na ujuzi, wale wasio na ujuzi, wauguzi, na huduma kwa wakongwe na walimu.

Mkutano huo pia uliarifiwa kuwa Wizara ya leba imepanga shughuli za mahojiano ya kazi katika kila kaunti, katika muda wa wiki zijazo.

Serikali imekuwa ikitafuta nafasi za ajira katika mataifa ya kigeni kwa raia wengi wa Kenya ambao wana ujuzi na utaalam mbali mbali.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article