Kenya ilianza vyema makala ya tatu ya mashindano ya Riadha kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18 na 20 barani Afrika kwa kuzoa dhahabu mbili Jumatano usiku uwanjani Mashood Abiola mjini Abeokuta, Nigeria.
Caren Jepchirchir alijizatiti na kushinda dhahabu ya mita 1500 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18, huku Lawi Ngétich pia akinyakua dhahabu ya mita 1500 kwa wavulana.
Nahodha wa kikosi cha Kenya Joyline Chepkemoi, aliridhia nishani ya fedha katika mita 3000.
Kenya inawakilishwa na wanariadha 47 huku mashindano hayo yakitarajiwa kukamilika Julai 20.