Timu ya taifa ya Raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande ukipenda Shujaa, itachuana na Fiji leo katika fainali ya Kombe mkondo wa Singapore Sevens.
Kenya imefuzu kwa fainali ya Singapore kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016, baada ya kuinyuka Uhispania pointi 12-5 katika semi fainali.
Patrick Odingo alifunga tries zote mbili huku Nygel Amaitsa, akiongeza conversion naye Pol Pla, akafunga try pekee kwa Wahispania.
Upande wao Fiji wameingia fainali kufuatia ushindi wa pointi 33-24, katika nusu fainali ya pili.
Fainali hiyo itakuwa marudio ya mwaka 2016, ambapo Shujaa iliwashinda Fiji ,na kutwaa kombe kuu kwa mara ya kwanza.
Shujaa wameshinda mechi zote tatu walizocheza kufikia sasa, huku wakiweka hai matumaini ya kusalia kwenye mashindano ya msururu msimu ujao.