Serikali ya Kenya imetia saini mkataba wa kibiashara na Muungano wa Ulaya, miongoni mwa nchi wanachama wa kundi la G7 Jijini Osaka Japan.
Mkataba huo utawezesha bidha za Kenya kuingia mwenye soko la mataifa 27 ya muungano huo bila kutozwa ushuru. Soko la Muungano wa Ulaya linakadiriwa kuwa la dola trilioni 18.
Waziri wa biashara Rebecca Miano, ambaye alikuwa waziri wa pekee wa biashara kutoka bara Afrika aliyealikwa kuhudhuria mkutano huo wa G7, alisema mchakato wa uidhinishwaji wa mkataba huo wa kibiashara, uko katika hatua za mwisho.
Katika kongamano hilo, waziri Miano pia alishiriki meza ya mazungumzo na naibu rais wa tume ya Ulaya Valdis Dombrovskis.
Muungano wa Ulaya na Kenya zimejitolea kuimarisha biashara baina yazo.
Kenya pia ilifanya mazungumzo ya pande mbili na shirika la biashara duniani WTO, Japan, India na Ufaransa.