Kenya yatambua Kosovo kuwa taifa huru

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 20 imetambua Kosovo kuwa taifa huru tangu kujitenga kwake.

Rais wa Albania Bejram Begaj, kupitia ukurasa wake wa X, alielezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo you Rais William Ruto kutambua Kosovo kuwa nchi huru.

Tangazo hilo lilifichuliwa na Balozi maalum wa Rais wa Kosovo humu nchini Behgjet Pacoli, alipokutana na Rais Ruto jijini Nairobi.

Hatua hii ina maana kuwa Kenya inatarajiwa kutambua rasmi pasipoti za Kosovo yenye idadi ya watu milioni 1.9, wengi wao wakiwa Waserbia na Waalbania.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *