Kenya yaripoti kisa cha tano cha Mpox

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya afya imethibitisha kisa cha tano cha virusi vya Mpox ambaye ni mwanfunzi wa umri wa miaka 28, katika mtaa wa VOK kaunti ya Mombasa.

Kulingana na Wizara ya afya mgonjwa huyo ni mke wa mgonjwa wa nne wa virusi hivyo.

Mgonjwa wa nne wa Mpox ametengwa katika hospitali ya Nakuru, huku mgonjwa wa hivi punde akitengwa katika hospitali ya Utange.

Sampuli 124 zimechunguzwa katika maabara kadhaa huku 110 zikitoa matokeo yanaoshiria kukosa virusi hivyo ihlai visa vingine tiza vinachunguzwa.

Wasafiri 687, 233 wamechunguzwa katika mipaka ya kuingia na kutoka Kenya kufikia sasa.

Wizara ya afya pia imethibitisha kuwa wawili kati ya wagonjwa watano wa Mpox, tayari wamepona baada ya kupokea matibabu.

TAGGED:
Share This Article