Rais William Ruto ameipongeza Algeria kwa kuisaidia sekta ya kilimo hasaa katika utoaji wa mbolea ya gharama nafuu.
Wakati huo huo Rais Ruto kupitia mtandao wa X, pia aliishukuru nchi hiyo kwa usaidizi wa kifedha kwenye mpango wa usalama unao-ongozwa na umoja wa mataifa nchini Haiti.
Rais Ruto aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa G7 na rais Tebboune Amadjid wa Algeria, Jijini Apulia, nchini Italia.
Rais huyo wa Algeria pia aliahidi kusaidia Kenya kwenye azma yake ya kuwania wadhfa wa mwenyekiti wa muungano wa Afrika.
Kenya na Algeria zinashirikiana kuleta mabadiliko kwenye mpango wa kifedha ili kuhakikisha kuna usawa.