Kenya yapokea vifaa vya kuchunguza ugonjwa wa Mpox

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya yapokea vifaa zaidi vya uchunguzi wa Mpox.

Kenya imepokea vifaa vya kuchunguza ugonjwa wa Mpox, kuhakikisha uchunguzi huo unatolewa kwa wakati na ni sahihi.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na shirika la misaada la Marekani na kusambazwa kupitia Shirika la Afya Duniani WHO, vitafanikisha kugunduliwa mapema kwa ugonjwa wa Mpox, na kudhibiti kuenea kwake hapa nchini.

Waziri wa afya Dkt. Deborah Barasa, alipokea vifaa hivyo katika makao makuu ya wizara hiyo leo Jumatatu asubuhi.

Hadi kufikia sasa Kenya imenakili visa 12 vya Mpox, huku visa vitano vikiendelea kuchunguzwa.

Visa hivyo vimeripotiwa katika kaunti ya Nakuru na Kajiado zikinakili visa 2, nazo kaunti za Taita Taveta, Busia, Mombasa, Bungoma, Kericho, Kilifi na Nairobi, zikinakili kisa kimoja kila kaunti.

Share This Article