Kenya yalenga kutumia umeme wa nyuklia kufikia 2038

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya inapania kuanzisha kiwanda cha kuzalisha umeme wa nyuklia ifikiapo mwaka wa 2038 kwa ushirikiano na mataifa ya Marekani, China na Korea Kusini.

Akizungumza katika mkutano kuhusu mpango huo jijini Nairobi siku ya Jumatatu, Mkurugenzi wa Maswala ya Sheria katika Shirika la Nishati ya  Nyuklia  nchini Justus Wabuyabo, alisema kuwa mradi huo baaada ya kuzinduliwa, unatazamiwa kurejesha gharama za matumizi baada ya takriban miaka 20, huku mitambo itakayotumika ikitarajiwa kudumu kwa miaka 80.

Mataifa hayo matatu pia yatawapa mafunzo wahandisi wa humu nchini jinsi ya kusimamia na kuhudumu katika mtambo huo wenye umeme mwingi.

Mpango huo ambao utagharimu shilingi billioni 500 na utakaozalisha umeme wa megawati 1,000, umekuwa na masharti mengi kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia, IAEA.

Kenya imeidhinishwa kuanzisha mpango huo baada ya kutimiza mengi ya masharti hayo na utanatarajiwa kuleta afueni kubwa hususan kupunguza gharama ya umeme.

lwapo Kenya itafaulu katika mpango huo, itakuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini kutekeleza matumizi ya nishati ya nyuklia.

TAGGED:
Share This Article