Kenya yajiunga na Ulimwengu kusherehekea siku ya uhuru wa uanahabari

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imejiunga na ulimwengu kusherehekea siku ya kimaraifa ya uhuru wa Wanabahari ambyo huadhimishwa kila Mei 3.

Kenya ni baadhi ya mataifa machache kote duniani yaliyo na uhuru  wa Wanahabari wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa,idadi ya mataifa yaliyopata uhuru kamili wa Wanahabari imepungua.

Ripoti hiyo inaelezea kuwa Uhuru wa Wanahabari umepungua nchini Uganda katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita,hali ikiwa sawa na hiyo nchini Kenya  ingawa Wanahabari wa kenya wanafurahia uhuru zaidi kuliko wenzao nchini Uganda.

Kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani (UNESCO),kinaandaa kongamano la uhuru wa vyombo vya habari mjini Santiago Chile.

 

Share This Article