Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande maarufu kama Shujaa, imejikatia tiketi kwa nusu fainali ya kombe kuu katika mkondo wa sita wa Singapore Sevens.
Kenya imeongoza kundi kundi B kufuatia ushindi wa pointi 17-7, dhidi ya Ireland, kabla ya kuilemea Ufaransa pointi 10-7.
Ni mara ya kwanza kwa Kenya kufuzu kwa semi fainali ya kombe kuu, huku wakifufua matumaini ya kusalia katika mashindano ya msururu endapo watafuzu kwa fainali.
Shujaa ilinyakua kombe kuu kwa mara ya kwanza na ya pekee hadi leo walipoinyuka Fiji, katika fainali ya mwaka 2016 ya mkondo wa Singapore