Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars iliweka hai matumaini ya kutwaa kombe la Mapinduzi, baada ya kuwacharaza Tanzania mabao mawili kwa nunge.
Brian Muchiri alipachika goli la kwanza kunako dakika ya 55, kabla ya Ryan Ogam kuongeza la pili dakika ya 67.
Ushindi huo unawaweka Kenya uongozini pa kundi la mashindano hayo kwa pointi 4 sawa na Burkina Faso.
Harambee Stars watahitimisha ratiba Ijumaa hii kwa mechi dhidi ya wenyeji Zanzibar.