Kenya yafuzu AFCON U 20 kwa mara ya kwanza

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 imefuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Burundi mabao 4-0, katika nusu fainali ya CECAFA iliyochezwa Ijumaa jioni katika uwanja wa Azam Sports Complex jijini Dares Salaam,Tanzania.

Lousi Ingavi,Hassan Beja,Aldrine Kibet na Lawrence Okoth  walipachika goli moja kila mmoja,huku Kenya ikifuzu kwa fainali ya kombe hilo kwa mara ya pili mtawalia.

Rising Stars itakumbana na  wenyeji Tanzania kwenye fainali ya Oktoba 20,yakiwa marudio baada ya Kenya kuilemea Tanzania 2-1, katika mchuano wa ufunguzi wa kundi A.

Tanzania ilijiakatia tiketi kwa fainali baada ya kuwabandua mabingwa watetezi Uganda Hippos mabao 2-1, katika muda wa ziada katika nusu fainali ya kwanza uwanjani KMC.

Kenya na Tanzania zimefuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao huku mwandalizi wake akitarajiwa kubainika kesho.

Share This Article