Kenya imebuni kikosi maaluma cha ulinzi kukabiliana na uchimbaji haramu wa madini nchini.
Katibu katika wizara ya madini Elijah Mwangi amesema kikosi hicho kitakabiliana na wale wanaovunja sheria zilizopo za uchimbaji madini.
Kulingana na sheria ulanguzi wa mihadarati ni kosa la jinai ambalo mhusika anatozwa faini ya shilingi milioni 1 au kifungo cha miaka 10 .
Serikali ya Rais William Ruto imefutilia mbali leseni 1,546 Oktoba mwaka uliopita kwa kukiuka sheria zinazothibiti uchimbaji madini.