Timu ya taifa ya voliboli ya wanaume ya Kenya maarufu kama Wafalme Stars ilianza vibaya mashindano ya kuwania kombe la bara Afrika walipotitigwa seti 3-1 na Cameroon jana Jumatatu usiku jijini Cairo, Misri.
Cameroon walitwaa seti mbili za mwanzo alama 25-22 na 25-20 kabla ya Kenya kujizatiti na kushinda seti ya tatu 26-24.
Hata hivyo, maji yalizidi unga kwa Kenya walipopoteza seti ya 25-17.