Kenya yaangukia kundi gumu kipute cha CHAN

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza Kenya wamejumuishwa kundi gumu la A, kwenye makala ya nane ya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu CHAN.

Katika droo hiyo iliyoandaliwa katika Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano KICC, jana usiku Harambee Stars ya Kenya imejumuishwa kundi A pamoja na mabingwa mara mbili DR Congo ,Morocco,Angola na Zambia.

Waandalizi wenza Tanzania wamo kundi B pamoja na Madagascar, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Waandalizi wenza wengine Uganda wataongoza kundi C pamoja na Niger na Guinea na timu nyingine mbili zitakazofuzu.

Maningwa watetezi Senegal wamo kundi la mwisho la D pamoja na Congo,Sudan na Nigeria.

Droo ya jana ilihudhuriwa na wachezaji nguli McDonald Mariga wa Kenya,Mrisho Ngasa kutoka Tanzania na Hassan Waswa wa Uganda.

Fainali za CHAN zitaandaliwa mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuahirishwa kutoka Februari.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *