Timu ya taifa ya soka Harambee Stars imerushwa kundi J, katika safari ya kufuzu kwa kipute cha AFCON mwaka 2025 nchini Morocco.
Kulingana ba droo iliyoandaliwa Alhamisi jioni nchini Afrika Kusini, Stars imo kundi J pamoja na mabingwa mara tano Cameroon na waakilishi wa ukanda wa COSAFA Zimbabwe na Namibia.
Kenya wataanza safari nyumbani kwa kuwaalika Zimbabwe,kabla ya kuizuru Namibia mwezi Septemba mwaka huu.
Oktoba mwaka huu Kenya itawazuru Cameroon na kuwaalika Indomitable Lions hao katika mchuano wa marudio.
Katika mechi mbili za mwisho Novemba mwaka huu ,Kenya watawaalika Namibia na hatimaye kuzuru Zimbabwe.
Makundi:
Group A: Tunisia, Madagascar, Comoros, Gambia
Group B: Morocco, Gabon,Central Africa Republic, Lesotho
Group C: Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana
Group D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda
Group E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia
Group F: Ghana, Angola, Sudan, Niger
Group G: Cote d’Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad
Group H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia
Group I: Mali, Mozambique, Guinea Bissau, Eswatini
Group J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe
Group K: South Africa, Uganda, Congo, South Sudan
Group L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi
Timu mbili bora kutoka kila kundi isipokuwa kundi B, zitafuzu kwa fainali za AFCON pamoja na timu moja ya kundi B.
Timu hizo 23 zitajiunga na wenyeji Morocco kwa makala ya 35 ya kipute cha AFCON, kati ya Disemba 21 mwaka ujao hadi Januari 18 mwaka 2026.