Kenya wakabiliana na Cameroon leo nusu fainali Voliboli ya vidosho Afrika

Kenya ambao wamehinda mechi zote  nne mashindanoni pia wanajivunia kupoteza seti moja pekee walipowazabua Algeria seti 3-1, katika hatua ya robo fainali.

Dismas Otuke
1 Min Read
Malkia Strikers

Wenyeji  Kenya watashuka katika ukumbi wa Kasarani Alhamisi usiku kwa nusu fainali ya mwisho dhidi ya Cameroon, kwenye mashindano ya kuwania Kombe la Afrika katika mpira wa wavu kwa wanawake Afrika.

Mechi hiyo itang’oa nanga saa moja usiku huku mshindi akijikatia tiketi kwa fainali ya Jumamosi hii.

Kenya ambao wamehinda mechi zote  nne mashindanoni pia wanajivunia kupoteza seti moja pekee walipowazabua Algeria seti 3-1, katika hatua ya robo fainali.

Cameroon nao waliibwaga Uganda seti 3-0 katika kwota fainali.

Share This Article