Kenya Pipeline wapakata vidosho wa DCI seti 3-1

Dismas Otuke
0 Min Read

Klabu ya Kenya Pipeline ilisajili ushindi wa seti 3-1 katika mechi ya kuwania taji la Kenya Cup.

Mchuano huo ulipigwa uwanjani Nyayo.

Pipeline walishinda  seti mbili za kwanza alama  25-17 na  25-16, ila wakapoteza ya tatu 24-26, na kuibuka kidedea katika seti ya mwisho  kwa alama 25-21.

Mechi hiyo ilikuwa ya raundi ya pili katika makala ya pili ya mashindano ya Kenya Cup.

Share This Article