Kenya Pipeline kukabana koo na Zamalek nusu fainali ya Afrika leo

Pipeline wamenyakua kombe la Afrika mara tano huku Zamalek wakitwaa ubingwa mara mbili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa Voliboli nchini, Kenya Pipeline, watachuana na mabingwa watetezi Zamalek ya Misri leo jioni katika nusu fainali ya Kombe la Afrika kwa wanawake mjini Abuja, Nigeria.

Pipeline ambao walipoteza mechi moja mashindanoni dhidi ya APR, watalenga kufuzu kwa fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2023 waliposhindwa na Zamalek.

Pipeline wamenyakua kombe la Afrika mara tano huku Zamalek wakitwaa ubingwa mara mbili.

Semi-fainali nyingine itakuwa kati ya Carthage ya Tunisia na Al Ahly ya Misri.

Waakilishi wengine wa Kenya, Prisons, watashuka uwanjani dhidi ya LTV ya Cameroon, wakati mabingwa wa Ligi KCB, wakipambana na APR kutoka Rwanda kuwania nafasi za 5 hadi 8.

Website |  + posts
Share This Article