Kenya na Venezuela kuimarisha diplomasia ya mabunge

Martin Mwanje
1 Min Read
Balozi wa Venezuela Moravia Peralta Hernandez akiwa na Spika wa Bunge la Taifa Moravia Peralta Hernandez

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula leo Alhamisi alikuwa mwenyeji wa Balozi wa Venezuela humu nchini Moravia Peralta Hernandez aliyemtembelea ofisini mwake kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na uhusiano wa mabunge ya nchi hizo mbili.

Wakati wa ziara hiyo, Hernandez aliwasilisha taarifa maalum kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Bunge la Taifa la Venezuela.

Taarifa ya Makamu huyo iliomba kubuniwa kwa Kundi la Urafiki wa Mabunge ya Kenya na Venezuela.

Kundi hilo linatarajiwa kuhamasisha diplomasia ya mabunge, mabadilishano ya kitamaduni na mazungumzo ya pande mbili kati ya Kenya na Venezuela.

“Bunge la Kenya  liko tayati kukuza uhusiano wenye tija kupitia diplomasia ya mabunge,” alisema Wetang’ula.

“Tunaunga mkono pendekezo hilo kutoka kwa marafaiki zetu kama ishara ya umoja na dhamira ya ushirikiano wa dunia.”

Wakat wa mkutano kati yao, viongozi hao wawili walibadilishana maoni juu ya masuala yanayoibuka ya kisiasa duniani, miundo ya bunge na nyanja za maslahi ya pamoja ikiwemo biashara, utalii na elimu.

Kwa upande wake, Balozi Peralta alisisitiza msaada endelevu wa Venezuela kwa masuala ya dunia, ikiwa ni pamoja na haki za watu wa Palestina na mipangokazi thabiti ya ushikiriano kati ya nchi zinazostawi duniani

 

Website |  + posts
Share This Article