Kenya na Uganda zasaini mwafaka wa uhifadhi mazingira

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya na Uganda zimesaini mwafaka wa kuimarisha uhifadhi mazingira kwa pamoja katika eneo la Suam,mpakani mwa nchi hizo mbili.

Hafla hiyo iliyoandaliwa katika eneo la Suam,mlima Elgon, iliwaleta pamoja maafisa wa serikali za Kenya na Uganda .

Eneo la mlima Elgon,lina ekari 74,000 za msitu unaojumuisha vyanzo vya mazji vinavyounganisha mito mitatu mikuu ya Nzoia, Turkwel na Malakisi, inayotegemewa na raia wa kenya na Uganda kwa maji ya matumizi ya kila siku.

Katibu wa mazingira aliyehudhuria hafla hiyo Gitonga Mugambi,alihimiza umuhimu wa hifadhi hiyo akiwaasa wakazi dhidi ya tabia kama vile ukati miti,na  mizozo ya binadamu na wanyama.

Uzinduzi wa hifadhi hiyo ulihudhuriwa na Makatibu Silvia Museiya wa wanayamapori,mwenzake wa Uganda Doreen ,balozi wa Kenya nchini Uganda Joash Maangi ,Afisa mkuu mtendaji wa shirika la Umoja wa mataifa la uhifadhi mazingira UNESCO afrika mashariki pamoja na waakilishi wa serikali za Kenya na Uganda.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *