Rais William Ruto amesema Kenya na Ufalme wa Milki za Kiarabu, UAE zinalenga kuimarisha ushirikiano wao wa kibiashara hata zaidi.
Huku akikiri kwamba nchi hizo mbili zinafurahia uhusiano mwema, kiongozi wa nchi alisema wanapania kuongeza bidhaa za Kenya zinazouzwa nchini humo hadi kiwango cha shilingi bilioni 34.6.
Aliyasema haya baada ya kukutana na kiongozi wa UAE Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, pembezoni mwa kongamano linaloendelea la mabadiliko ya tabia nchi almaarufu COP28.
Rais Ruto anahudhuria kongamano hilo akiwa ameandamana na viongozi kadhaa serikalini.
Alifanya mazungumzo pia na Rais wa Kosovo, Vjosa Osmani ambapo walikubaliana kushirikiana katika masuala kadhaa ya manufaa kwa nchi zote mbili.