Kenya na Morocco zasaini mikataba 11 ya ushirikiano

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya na Morocco zimetia saini mikataba 11 ya ushirikano kwa manufaa ya mataifa hayo  mawili.

Mikataba hiyo ilisainiwa jana katika kikao cha kwanza cha pamoja cha Mawaziri jijini Nairobi .

Ushirikiano huo ni wa sekta za;kilimo,afya,elimu ya juu,uchumi wa baharini,uvuvi,ufugaji wa viumbe wa majni,haki na sheria,jinsia na uwezeshaji wanawake,utamaduni,misaada ya masomo na mafunzo ya nyanjani,michezo,uhamiaji,usimamizi wa wanyamapori na kubadilishana maarifa.

Pia mataifa hayo mawii yalikubaliana kuharakisha kubuni mwafaka wa  ushiriakiano katika sekta za biashara,uwekezaji,ukuzaji wa viwanda na usafiri wa angani ii kubuni nafasi na fursa za kimaendeleo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na kinara wa mawaziri  Musalia Mudavadi pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Morocco Nasser Bourita.

Mawaziri wa Kenya waliohudhuria kikao hicho na kushuhudia utiaji sahihi za ushirikiano ni, Aden Duale wa Afya, Julius Migos Ogamba wa elimu pamoa Hannah Cheptumo wa jinsia .

Share This Article