Kenya na India zaimarisha ushirikiano wa kibiashara

Dr. Yusuf Muchelule
1 Min Read
Kenya na India zaimarisha ushirkiano wa kibiashara.

Katibu katika wizara ya kilimo Dkt. Kipronoh Ronoh, amesema Kenya imejitolea kuimarisha biashara kati yake na India, kwa ustawi wa nchi hizo mbili.

Dkt. Ronoh, alisisitiza haja ya ushirikiano dhabiti wa kiuchumi hasaa katika sekta za Majani Chai, Sukari, Teknolojia na Uvumbuzi, akisema Kenya itahakikisha ushirikiano huo unafaulu.

Aliyasema hayo Alhamisi asubuhi, alipokutana na ujumbe wa kundi la wafanyabiashara wa India, ambao unazuru taifa hili kwa shughuli za kibiashara kuanzia Februari 18 hadi 21.

“Majadiliano yetu yalizingatia upanuzi wa fursa za uwekezaji katika sekta muhimu, zikiwemo Kilimo, Dawa, Elimu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, utalii na Utengenezaji bidhaa,” alisema Dkt. Ronoh.

Huku akielezea azma ya Kenya ya kuimarisha biashara na uwekezaji na India, Dkt. Ronoh alisema, “Kenya na India zina ushirikiano dhabiti na ni wanachama wa Jumuiya ya Madola pamoja na taasisi zingine za kimataifa,”.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *