Kenya na China zafanyia kazi makubaliano ya biashara

Makubaliano ya biashara kati ya nchi hizo yanakusudia kupanua upatikanaji wa soko hasa kwa bidhaa za Kenya zinazouzwa nje ya nchi kama vile majani chai na kahawa wakati pia yakihamasisha ushirikiano mkubwa wa kiuchumi.

Martin Mwanje
1 Min Read
Katibu wa Biashara Regina Ombam akiwa na Balozi wa China nchini Kenya, Guo Haiyan. 

Kenya na China zinafanyia kazi makubaliano ya biashara ya awali yanayolenga kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Hayo yamebainika wakati wa mkutano kati ya Katibu wa Biashara Regina Ombam na Balozi wa China humu nchini, Guo Haiyan.

Wakati wa mkutano kati yao, wawili hao walizungumzia hatua iliyopigwa kuelekea kufikiwa kwa makubaliano hayo.

Aidha, mazungumzo kati yao yaliangazia hatua za usafi wa bidhaa za samaki na kilimo ili kufanikisha biashara na kuhakikisha kuzingatiwa kwa viwango vya kimataifa.

 

 

Makubaliano ya biashara kati ya Kenya na China yanakusudia kupanua upatikanaji wa soko hasa kwa bidhaa za Kenya zinazouzwa nje ya nchi kama vile majani chai na kahawa wakati pia yakihamasisha ushirikiano mkubwa wa kiuchumi.

 

Pande zote pia zilisisitiza dhamira yao ya kukuza ushirikiano wenye manufaa ya pande mbili unaounga mkono biashara endelevu, uwekezaji na ustawi wa pamoja.

 

Website |  + posts
Share This Article