Kenya na taifa la kisiwa cha Bahamas zimekubaliana kuanzisha ubalozi katika miji ya Nairobi na Nassau kwenye juhudi mpya za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia.
Waziri mwenye mamlaka makuu aliye-pia waziri wa mashauri ya mambo ya nje Musalia Mudavadi, amesema hatua hiyo itatoa nafasi ya biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili.
Wakati wa mkutano baina ya Mudavadi na waziri wa uhamiaji wa Bahamas Alfred Sears, makubaliano yaliafikiwa kwamba mataifa hayo mawili yataharakisha mchakato huo ili kuhakikisha kwamba mpango mzima wa kuwa na mabalozi baina ya mataifa hayo unafanikiwa.
Hayo yaliafikiwa pembezoni mwa mkutano wa 19 wa mawaziri unaoendelea jijini Kampala nchini Uganda.
Mudavadi alielezea matumbaini kuhusu makubaliano hayo akisema mataifa hayo yanalenga uhusiano mwema na dhabiti.
Sears kwa upande wake alisema Bahamas imejitolea kuboresha uhusiano wake na jamii ya kimataifa na kwamba imetambua kenya kuwa kutovu cha biashara cha eneo la afrika mashariki na kati na bara nzima.