Kenya miongoni mwa mataifa10 yatakayopokea mgao wa pesa za kukabiliana na tabia nchi

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya ni miongoni mwa mataifa 10 yatakayopokea nusu ya kitita cha shilingi bilioni 100 zilizotengewa bara Afrika kwa vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mataifa mengine yatakayonufaika na kitita hicho ni Misri, Morocco, Nigeria, Ethiopia, Afrika Kusini, Msumbiji , Cote d’Ivoire, Tunisia na Ghana, kwa mjibu wa kongamano la kwanza la Afrika kuhusu tabia nchi linaloandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano ya kimataifa, KICC.

Nchi 10 za Afrika zinazokabiliwa na makali ya mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na Guinea-Bissau, Sierra Leone, South Sudan, Nigeria, DRC, Ethiopia, Eritrea, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad na Senegal huku zikitengewa asilimia 18 ya pesa  hizo.

Kulingana na Wizara ya Mazingira, Kenya inahitaji angalau dola bilioni 40 za Marekani kuwekeza ili kukabiliana na tabia nchi.

Shirika la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi lenye makao yake nchini Uholanzi limedokeza kuongeza mgao wa pesa zinazotolewa kwa mataifa ya Afrika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi  hadi mara 10 ifikiapo mwaka 2035.

Share This Article