Kenya itashuka uwanjani mapema kesho katika mchuano wa kuwania nafasi ya tisa dhidi ya Afrika Kusini,katika msururu wa dunia wa Hon Kong Sevens .
Shujaa walisajili ushindi mmoja pekee pointi 19-0 dhidi ya Uhispania jana, kabla ya kushindwa na Uingereza 12-7, na hatimaye kulemewa na Ufaransa 14-7 mapema leo katika mechi za kundi C.
Katika nusu fainali ya kuwania nafasi ya tisa Kenya wameishinda Marekani alama 17-10.
Kenya ni ya tisa katika msimamo wa dunia kwa pointi 15 baada ya misururu minne.