Kenya kutuma polisi 600 zaidi nchini Haiti

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya inapanga kutuma kundi la pili la maafisa wa polisi 600 nchini Haiti kuimarisha usalama .

Haya yamesema na Rais William Ruto alipokutana na Waziri Mkuu wa Haiti Dkt.Garry Conille, aliye kwenye ziara ya siku nne nchini katika Ikulu ya Nairobi siku ya Ijumaa.

Hali ya usalama imekuwa tete nchini Haiti baada ya magenge ya majangili kuvamia sehemu za Kaskazini mwa nchini hiyo, huku takriban watu 70 wakiuawa wakiwemo wanawake,wanaume na watoto.

Ruto amesema wamekubaliana kushirikiana ili kuimarisha biashara na kukuza mbinu za uekezaji kati ya Kenya na Haiti.

“Licha ya hatari, tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa wanajeshi wanaoshiriki wanalindwa vyema.” Conille.

Aidha, walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana na kutoa usaidizi kwa maafisa wa usalama walio Haiti.

TAGGED:
Share This Article