Kenya kutanua ushirikiano wa kiabiashara na Marekani

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na kuafikiana kutanua biashara baina ya Kenya na Marekani.

Ruto na Rubio wamekutana mapema Alhamisi mjini New York Marekani,pembezoni mwa kongamano la 80 la Umoja wa Mataifa-UNGA.

Aidha, Kenya na Marekani zimekubaliana kukamilisha mwafaka wa kibiashara kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, kuongeza biashara za Marekani nchini Kenya, na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiusalama, hususan vita dhidi ya ugaidi.

Rubio pia amepongeza mchango mkubwa wa Kenya katika kuimarisha usalama katika kanda ya Afrika Mashariki.

Website |  + posts
Share This Article