Kenya kushirikiana na Serbia kuimarisha michezo na uchumi bunifu

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya na Serbia zitaharakisha utiaji saini wa mwafaka wa makubaliano yanayolenga kuimarisha sekta za michezo, sanaa na uchumi bunifu kwa vijana.

Haya yameafikiwa jana baina ya Waziri wa michezo, masuala ya vijana na uchumi bunifu Salim Mvurya, pamoja na Balozi wa Serbia nchini Kenya, Danijela Cubrilo, aliyemtembelea ofisini.

“Tunataka kuunganisha shughuli za michezo kama vile soka, voliboli, mpira wa kikapu, mashindano ya maji ili kuwaruhusu wanariadha wa Serbia, kufanya mazoezi katika nyanda za juu humu nchini,” akasema Mvurya.

Upande wake Balozi Cubrilo, amesema watatumia ushirikiano huo na Kenya kuwakuza wanariadha wake.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *