Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande ya wanaume ukipenda Shujaa ,itarejea kucheza dhidi ya Samoa Jumamosi jioni katika siku ya nne ya michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa.
Mchuano huo utakuwa wa kuwania nafasi za 9 na 10 kuanzia saa kumi na mbili kamili.
Kenya watalenga ushindi ili kudumisha nafasi ya 9 waliyoafikia katika Olimpiki ya mjini Tokyo mwaka 2021, na kulipiza kisasi cha kucharazwa na Samoa pointi 26-0, katika mechi ya mwisho ya kundi hapo juzi.
Katika mechi za nusu fainali za leo Afrika Kusini itapambana na wenyeji Ufaransa kuanzia saa kumi unusu,kabla ya mabingwa watetezi Fiji kumaliza udhia na Australia saa kumi na moja jioni.