Kenya kukwangurana na Tanzania CECAFA U-20

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imepangwa katika kundi moja la A na wenyeji Tanzania katika mashindano ya kuwania kombe la CECAFA kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20.

Mataifa mengine kundini A pamoja na Kenya ni Sudan, Rwanda na Djibouti.

Mabingwa wa kombe hilo mwaka 2022 Uganda wamerushwa kundi B pamojana Sudan Kusini, Burundi na Ethiopia.

Mashindano hayo yataandaliwa katika viwanja vitatu vya Azam Complex, KMC na Major General Isamuhyo, vyote vilivyo jijini Dar es Salaam,Tanzania.

Michuano hiyo itakayotumika kutafuta mwakilishi wa CECAFA katika fainali za AFCON kwa chipukizi itaandaliwa kati ya Oktoba 6 na 20 mwaka huu.

Timu mbili bora michuanoni zitafuzu kuwania kombe la AFCON mwaka ujao.

Share This Article