Timu ya taifa ya raga ya Kenya ya wachezaji saba upande itashuka uwanjani leo kwa mechi ya mwisho na ya kufa kupona dhidi ya Samoa, katika siku ya pili ya michezo ya Olimpiki jijini Paris,Ufaransa.
Mchuano huo wa kundi B utang’oa nanga saa tisa alasiri, huku atakayeshinda akiweka hai matumaini ya kuikatia tiketi ya robo fainali, baada ya kushindwa mechi mbili za ufunguzi kundini B jana .
Kenya ilipigwa pointi 31-12 na Argentina katika mechi ya ufunguzi ,kabla ya kulemewa na Australia alama 21-7 katika mechi ya pili.
Samoa kwa upande wake ilicharazwa 21-14 na Australia na pia kulazwa 28-12 na Argentina katika mechi ya pili jana.