Kenya kukosa mwakilishi wa ligi ya mabingwa Afrika kwa mwaka wa pili

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya haitakuwa na mwakilishi katika mashindano ya kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika,kufuatia kutimuliwa kwa mabingwa wa ligi Gor Mahia kwa ukiukaja wa sheria za FIFA.

Sawia na mwaka jana wakati Kenya ilikuwa inatumikia marufuku,kwa mwaka wa pili mtawalia mabingwa wa ligi ya Kenya hawatashiriki kipiute hicho.

Shiirkisho la kandnanda Afrika CAF linaonekana kutupilia mbali ombi la FKF, waliopendekeza nafasi ya Gor Mahia ipewe Tusker FC waliomaliza wa pili ligini.

Masaibu ya Kogalo yalianza baada ya kukosa kuwalipa wachezaji watatu wa kigeni malimbikizi ya mishahara yao ndani ya makataa waliyopewa na FIFA.

Kulingana na orodha iliyotolewa Jumapili,Kenya itawakilishwa na Kakamega Homeboyza katika kombe la shirikisho ambalo droo yake sawia na ile ya ligi ya mabingwa itaandaliwa Jumanne Julai 25.

CAF imefanya mabadiliko kadhaa katika kombe la ligi ya mabingwa na lile la shirikisho, ambapo kutakuwa na mchujo mmoja pekee kabla ya kupisha hatua ya makundi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *