Kenya itajiunga na ulimwengu kusherehekea siku ya kiamtaifa ya usafi leo huku siku hiyo ikilenga kuhamasisha, kuhusu umuhimu wa kuokota taka na kudumisha mazingira safi.
Sherehe hiyo itaongozwa na mamlaka ya usimamizi wa mazingira nchini NEMA katika bustani ya Michuki jijini Nairobi.
Kaulimbiu ya sherehe za mwaka huu ni buni nafasi ya maisha,tumalize uharibifu.
Siku hii husherehekewa kila Septemba 20 tangu ibuniwe na kikao kikuu cha Umoja wa mataifa UNGA .
Jumla ya watu milioni 19.1 walishiriki katika usafishaji wa mazingira kwenye maadhimisho ya mwaka jana, mataifa 198 yakishiriki na taka tani 219 zikikusanywa.